RAIS wa Liberia George Weah amekubali kushindwa katika uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika wiki hii.
Weah amepigwa kumbo na kiongozi wa upinzani Bwa. Joseph Boakai baada ya ushindani mkali wa urais.
Boakai, makamu wa rais wa zamani ambaye alishindwa na Weah katika uchaguzi wa 2017, aliongoza kwa asilimia 50.9 ya kura dhidi ya Weah 49.1%, huku takriban kura zote zikiwa zimehesabiwa, tume ya uchaguzi nchini humo ilisema Ijumaa.
“Muda mfupi uliopita, nilizungumza na Rais mteule, Joseph Boakai kumpongeza kwa ushindi wake, mawaomba muige mfano wangu wa kukubali matokeo ya uchaguzi." alisema Weah alipohojiwa na Redio ya Taifa ya nchi hiyo.
0 Comments