Ticker

7/recent/ticker-posts

USHINDI WA YANGA WAMSABABISHIA KIFO, APIGWA MARUNGU AKIDHANIWA NI MWIZI

Ushindi wa bao 5-1 iliyoupata timu ya Yanga umedaiwa kusababisha kifo cha mfanyabiashara wa vifaa vya pikipiki anaeendesha biashara zake  katika eneo la mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilayani Geita, Alex Mayaya (40).

Mayaya amekutana na kifo baada ya  kupigwa na walinzi wa dukani kwake waliodhania kuwa ni mwizi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Safia Jongo amethibitisha taarifa hiyo na kueleza tukio lilitokea usiku wa kuamukia siku ya jumatatu ya Novemba 6, 2023.

Amesema Mayaya ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa ni shabiki wa timu ya Yanga na baada ya ushindi dhidi ya watani zao Simba alishangilia kwa kulewa na marafiki na kisha akarejea dukani kwake.

“Baada ya ushindi ule wa Yanga alishangilia kupita kiasi na akanywa pombe nyingi, akiwa amelewa  akaenda kwenye duka lake lililopo eneo la Kilimahewa, Katoro wilaya ya Geita”

“Alifungua duka akachukua matairi mawili ya pikipiki kwani huyo mfanyabiashara alikuwa anauza spea za pikipiki lakini kwa bahati mbaya hilo duka linaendeshwa na kijana wake”

“Wale walinzi hawamfahamu vizuri kwa hiyo wakahisi ni mwizi kwa hiyo baada ya kuhisi ni mwizi walimkamata, na kumshambulia kwa kumpiga na rungu.”

Ameeleza kipigo cha rungu kiligusa eneo la mshipa mkubwa wa damu hali iliyomsababisha maumivu makali kwa  na ilipofika asubuhi ya Novemba 6, 2023 mauti yakamkuta.

“Wananchi wanaomfahamu waligundua yule siyo mwizi, isipokuwa ni mwenye duka, kwa hiyo wakampeleka kituoni akapewa PF3, lakini alipofikishwa hospitali alifariki muda mfupi baadaye.

Post a Comment

0 Comments