Ticker

7/recent/ticker-posts

WABUNGE WAMPOKEA PROF JAY KWA KISHINDO

Aliyekuwa Mbunge wa Mikumi na Mwenyekiti wa Professor Jay Foundation ambaye pia ni mwanamuziki, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay, jana amepokelewa kwa kishindo na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jay alikwenda bungeni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Foundation hiyo Blackchatta (Black Rhino).

Wawili hao walifika Bungeni Jijini Dodoma kwa mwaliko maalum wa Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU),Dkt. Tulia Ackson.

Post a Comment

0 Comments