Ticker

7/recent/ticker-posts

TASAC KUTENGENEZA BOTI TANO ZA UOKOZI

SHIRIKA la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeanza kutengeneza boti tano za uokozi.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 5,2023  na Kaimu Mkurugenzi wa TASAC Nelson Mlali, jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na wahariri wa vyombo vya habari katika vikao kazi vinavyoendelea chini ya uratibu wa  ofisi ya Hazina kwa lengo la kuleta uelewa wa pamoja kwa wananchi juu ya Utendaji wa  mashirika na taasisi za serikali. 

Mlali ameweka wazi kuwa Shirika hilo linatekeleza miradi mikubwa mitatu ukiwemo mradi wa Ujenzi wa boti tano za uokozi  ambazo zikikamilika zitagaiwa katika maziwa matatu nchini ambayo ni Ziwa Victoria  ambako watapatiwa boti mbili, Ziwa Tanganyika pia boti mbili na Ziwa Nyasa watapatiwa boti moja.


Aidha, ameainisha miradi mengine miwili kati ya hiyo mitatu, ambayo ni

Mradi wa Kimataifa wa Mawasiliano na

Uchukuzi katika Ziwa Victoria (Multi-National Lake Victoria Maritime Communication and Transport- MLVMCT) unaotarajiwa

Kukamilika mwezi Desemba, 2024 pamoja na mradi wa Uendelezaji na Uimarishaji wa Miundombinu na Mifumo ya TEHAMA.

Post a Comment

0 Comments