Sare ya 2-2 iliyoipata timu ya Simba kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League ( AFL) dhidi ya Al Ahly imetazamwa kama chachu ya ushindi kwenye mchezo wa marudiano.
Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira amesema ameridhishwa na kile kilichofanywa na wachezaji wake kwenye mchezo huo kwani wameweza kutoka nyuma na kuuchukua mchezo.
Robertinho amesema anaamini chochote kinaweza kutokea katika mchezo wa marudiano utakaopigwa nchini Misri.
Kwa upande wake kiungo mshambualiaji wa Simba Saido Ntibazonkiza amesema wachezaji wamefanya kile ambacho walipaswa kukifanya na bado wanaaamini wana uwezo wa kuiondosha Al Ahly kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya Vilabu Afrika.
Nyota wa Al Ahly, Percy Tau amesema ameridhishwa na matokeo ya mchezo huo kwani Simba walirudi imara zaidi kwenye kipindi cha pili.
Kwa matokeo hayo Simba ili itinge nusu fainali ya AFL inahitaji ushidi wa aina yoyote nchini Misri au sare ya kuanzia mabao matatu.
0 Comments