Polisi wamepiga marufuku mashabiki wa soka wanaoendelea kujitokeza kwa wingi kutaka kushuhudia mchezo wa ufunguzi wa michuano ya African Football League kuingia uwanjani na chupa za maji.
Leo Tanzania inaweka historia ya kuwa nchi ya kwanza Afrika kuzindua michuano hiyo mipya ya ngazi ya klabu barani humu, ambapo timu ya Simba itamenyana na Al Ahly ya Misri.
Hatua hiyo ya kupiga marufuku mashabiki kuibgia na maji uwanjani imeonekana kuwashtua mashabiki lakini wameelewa baada ya kupewa maelekezo ya kina na polisi waliosimama vyema katika kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao.
Hakuna aliyebisha baada ya kuambiwa kufanya hivyo walitekeleza na kuingia ndani kwa utaratibu mzuri.
Mbali na hilo, lakini pia eneo la mageti ambalo mashabiki husimama kwa ajili ya kuingia ndani ya uwanja nalo limezungushwa vyuma lengo likiwa ni kuepusha msongamano kutokana na ukubwa wa mchezo wenyewe.
Licha ya kuwekewa vizuizi hivyo mashabiki wamekuwa watulivu na kufuata taratibu wakiingia kwa mstari.
0 Comments