Rais Samia Suluhu Hassan ametoa siku 180 kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Gissima Nyamo-Hinga kuhakikisha nchi inaondokana na suala la kukatika katika kwa umeme.
Rais Samia alimtaka Hinga kuendeleza pale alipoishia mrithi wake Maharage Chande.
"Mkurugenzi mpya wa TANESCO nenda kaanzie pale Maharage alipofikia, najua utaweza, nakupa miezi sita nakuangalia pale, kazi yako ya kwanza ni kusimamia ukarabati wa mitambo ya umeme, lakini baada ya miezi sita nisisikie kelele tena za kukatika kwa umeme," alisema Rais Samia.
0 Comments