Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekuwa ukipata Hati Safi (unqualified reports), kwa mujibu wa taarifa za mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) hali inayothibitisha usalama wa fedha za wanachama katika mfuko huo.
Hata hivyo mfuko umeendelea kuimarisha mifumo na usimamizi wa fedha ili kuepuka mianya ya upotevu wa fedha, kuendelea kumudu gharama za uendeshaji pamoja na kulipa mafao stahiki kwa wastaafu na wanufaika wengine.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa NSSF, Masha Mshamba, Septemba 25, 2023 katika kikao kazi na Wahariri wa Vyombo vya Habari kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam
0 Comments