Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira kitengo cha Mabadiliko ya Tabianchi Tathmin ya Mazingira, Deogratius Paul, akifungua rasmi kikao cha wataalamu |
NA JIMMY KIANGO- AFRINEWS, JET- DODOMA
OFISI ya Mkamu wa Rais (ORM) kwa kushirikiana na Shirika la umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) inatekeleza mradi wa kujenga uwezo wa utayari wa nchi katika kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi huo unahusisha kuandaa mpango wa Kitaifa wa kuhuisha masuala ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi katika mipango ya nchi iliyopewa jina la National Adaptation Plan (NAP).
Katika kufanikisha mpango huo Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa kikao cha wataalamu kwa ajili ya kupitia na kuridhia taarifa mbili za mradi huo ambazo ni Mwongozo wa kufundisha kwa wataalamu mbalimbali nchini ili kuwajengea uelewa wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
Sanjari na hilo pia kikao hicho kilichofanyika kwa siku mbili Septemba 14-14, 2023 jijini Dodoma kililenga kupitia taarifa ya Mkakati wa Utekelezaji wa Mradi huo (NAP Framework).
Mtaalamu wa mazingira kutoka UNDP, Felister Lukuka, akitoa neno la shukurani wakati wa zoezi la ufunguzi wa kakao cha wataalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi. |
“Hii si changamoto ya mtu mmoja, ni changamoto ya dunia na inaathiri sekta mbalimbali, ni jukumu letu sisi sote kuhakikisha elimu sahihi inawafikia wananchi popote walipo.
“Nikipongeze kikosi kazi kwa kazi nzuri ya kuandaa taarifa hizi mbili, si jambo dogo kufanikisha jukumu hili, nawaahidi serikali itaendelea kulitilia mkazo suala hili ili kuhakikisha tunakuwa na utayari wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Paul.
Kwa upande wake mwakilishi wa UNDP kwenye kikao hicho ambaye pia ni mtaalamu wa mazingira wa shirika hilo, Felister Lukuka, alisema ni furaha kwao kuona Tanzania imechukua uamuzi sahihi wa kutafuta namna nzuri ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi.
“UNDP imefurahishwa na hatua hii na tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kila hatua ya mradi huu.”
Mratibu wa mradi huo Bi. Asia Akule akitoa neno kwa washiriki wa kikao hicho, hawapo pichani. |
Haha ni baadhi ya washiriki wa kakao hicho |
0 Comments