Hatua ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuifungua nchi kiuchumi imemkuna
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Ephraim Mafuru.
Katika kuonesha manufaa ya hayo, Mafuru hakuficha hisia zake, alizielekeza shukurani zake kwa Rais Samia na kumuomba aendelee na uamuzi wake huo.
Mafuru ameyasema hayo Leo, Septemba 14,2023 kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha JNICC, kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo ni muendelezo wa vikao kazi vya Taasisi na Mashirikia ya Umma vinavyoraribiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Mafuru amesema juhudi za Rais Samia zimesababisha kituo hicho kuwa kitovu cha diplomasia ya uchumi inayochagizwa na mikutano ya Kimataifa inayofanyika nchini.
"Kufanyika kwa mikutano ni hatua inayochangia kuimarisha shughuli za kiuchumi na kukuza pato la Taifa."
Aimeongeza kuwa,kwa sasa wageni wanaipenda Tanzania na wanakuja kwa wingi, hii ni kutokana na juhudu za Rais za kuifungua nchi kiuchumi.
“Ninajua kuna Royal Tour, lakini pia amekuwa akishiriki mikutano mbalimbali yenye kuitangaza nchi, hiyo imesaidia kuitangaza Tanzania na kuwa chaguo muhimu na kuvutia mikutano mbalimbali ya Kimataifa”.
0 Comments