Ticker

7/recent/ticker-posts

​STAMICO YAKUZA PATO LA NDANI, SASA KUANZISHA BENKI YA WACHIMBA MADINI

Na. Jimmy Kiango- Afrinews DSM

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limefanikiwa kukuza pato lake la ndani kutoka shilingi bilioni 1.3 mwaka 2018/19 hadi kufikia shilingi bilioni 61.1 mwaka 2022/23.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, CPA Dkt. Venance Mwase alipokutana na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini pamoja na waandishi wa Habari leo Agosti28,2023.

Dkt. Mwase alisema moja ya mambo waliyofanikiwa kama shirika ni kuhakikisha linatoka kuwa shirika lenye kutengeneza hasara na kuwa shirika linalotengeneza faida, jambo ambalo wamefanikiwa.

Amesema sasa wamekuwa wakilipa gawio la jumla uya shilingi bilioni nane serikalini na kwamba wameondokana kabisa na utegemezi ruzuku kutoka serikalini

Aidha wameondokana na mwenendo wa kupata hati chafu kutoka kwa Mkaguzi na Madhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)na badala yake wamekuwa wakipata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo sasa.

Pamoja na mafanikio hayo, lakini pia kwa mwaka huu wa 2023 wamefanya uwekezaji mkubwa kwa kununua vifaa na mitambo mbalimbali ya kuchimba, kuchoronga na kuchenjua madini yenye thamani ya shilingi bilioni 17.8.


Shirika hilo ambalo lina kandarasi tatu kubwa za uchorongaji zenye thamani ya shilingi bilioni 55.2 pamoja na mafanikio mbalimbali ikiwemo kuwa sehemu ya kuongeza wigo wa ajira kwa Watanzania pia imepata sifa ya kuwa na utendaji bora unaozingatia masuala ya usalama katika shughuli za uchorongaji ndani ya GGM. 

Shirika hilo limekuwa likisaidia kwa kiasi kikubwa kuwaendeleza wachimbaji wadogo, ambapo liliwahi kufanya utafiti kwa wachimbaji hao na kubaini kuwa pamoja na fursa wa kisheria, lakini wanachangamoto ya elimu ya uchimbaji, ukosefu wa taarifa sahihi za mashapo, teknolojia duni, kutokuwa na mtaji na kutokopesheka na ukosefu wa masoko ya bidhaa zao.

Katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanakopesheka shirika limeingia makubaliano na taasisi za fedha hasa benki za CRDB, NMB,AZANIA na KCB ili ziweze kuwakopesha mitaji FEMATA na shirika limeanza taratibu za kuanzisha benki ya wachimbaji nchini.

Katika upande wa kuhakikisha wachimbaji wadogi wanakuwa na vifaa vya uhakika vya kufanyia kazi zao, STAMICO imeingia makubaliano na kampuni za GF Truck na Apolo pamoja na kuwakutanisha wachimbaji wadogo wa madini ya viwandani (DACOREMA) na wenye viwanda.


Katika kuhakikisha shirika linaendelea kuimarika wamejipanga kuondokana kabisa na utegemezi wa mishahara kutoka serikalini kuanzia mwaka 2024/25.

Kuongeza gawio serikalini mwaka 2024/25, kuzalisha kwa wingi mkaa mbadala wa Rafiki briquetters unaotokana na makaa ya mawe, kuimarisha uchimbaji mkubwa wa makaa yam awe, kuongeza uwekezaji wake kwenye tasnia ya uchorongaji, kuendeleza leseni za shirika na kuzitangaza kwa lengo la kupata wawekezaji wa madini ya kimkakati ya lithium, graphite, Ree na Copper  na kutekeleza mpango wa utafiti wa leseni za shirika.

Post a Comment

0 Comments