Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus, imeeleza kuwa Balozi Siwa ameapishwa leo Agosti 28,2023, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi Siwa amechukua nafasi ya Bw. Said Hussein Massoro ambae ameteuliwa kuwa Balozi.
0 Comments