Bunge limetoa rai kwa wabunge wake kutouingiza bungeni mjadala wa mkataba wa Bandari kati ya serikali ya Tanzania na Dubai na badala yake waendelee kusikiliza maoni ya wananchi.
Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson leo bungeni jijini Dodoma,amewataka wabunge waendelee kusikiliza maoni mbalimbali yanayotolewa na wananchi, lakini upande wao kuzungumza suala hilo bungeni ulishapita na Bunge tayari lilimaliza kazi yake.
Hata hivyo amesema kwa vile kazi ya Bunge ni kuishauri na kuisimamia serikali, inaweza kufanya hivyo pale serikali itakapoleta hoja zake bungeni kuhusu suala la mikataba itakayoingia.
Kutokana na hali hiyo, Dk Tulia amewataka wananchi wasihofu, kwani kazi ya Bunge ni kuishauri na kuisimamia serikali, hivyo ikiletwa bungeni hoja kuhusu mikataba wanayoingia, Bunge litafanyia kazi na kuishauri serikali.
0 Comments