Ticker

7/recent/ticker-posts

​​​TRA YAZINDUA KAMPENI YA MATUMIZI SAHIHI YA EFD KARIAKOO


​​​Na. MWANDISHI WETU, Afrinews DSM

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi wa Kariakoo imezindua kampeni maalum kwa ajili ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mashine za kieletroniki (EFD) kwa wafanyabiashara nchini.

Kampeni hiyo imeambatana na ubandikaji wa stika maalum za kuhamasisha wafanyabiashara kutoa risiti pale wanapouza bidhaa zao na wananchi kudai risiti ambayo itakuwa thamani sawa na bidhaa waliyonunua kwa maendeleo ya taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 29,2023 jijini, Dar es Salaam, Meneja Msaidizi  wa ukaguzi TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Thoddy Beyanga amesema kuwa  wamebaini kuporomoka kwa utoaji wa risiti kwa sababu zinazotolewa zimekuwa tofauti na matarajio  na kusababisha kushuka kwa makusanyo kushuka.

Beyanga amefafanua kuwa faida za kutoa na kudai risiti pale biashara inapofanyika husaidia  kutunza kumbukumbu na katika ukadiliaji wa mapato yanayoendana na uhalisia wa biashara pamoja na kuchangia pato la taifa.

Amesema kampeni ya uhamasishaji wa wafanyabiashara kutoa risiti na wananchi kudai risiti ni endelevu hivyo jamii inatakiwa kutekeleza bila shuruti.

Post a Comment

0 Comments