Uongozi wa klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia, umetishia kuvunja mkataba na kocha wake Nuno EspÃrito Santo endapo mshambuliaji wa kimataifa, Karim Benzema ataacha kwenda mazoezini. Tishio hilo linatokana na kauli za Santo za hivi karibuni kuwa hafurahishwi na uchezaji wa mshambuliji huyo kulingana na aina yake ya uchezaji na anadai kuwa hakuwahi kuomba kusajiliwa kwa mchezaji huyo klabuni hapo.
Benzema alimwambia Saad Al-Ladidh ambaye aliweza kumshawishi Benzema kujiunga na klabu hiyo kwamba hakuridhika na uwamuzi wa kocha Nuno EspÃrito.
Benzema alikuwa ameomba kitambaa cha unahodha lakini kocha akampa Romarinho, hivyo Benzema hakwenda mazoezini leo asubuhi (Jumatano).
Kocha Nuno anaikosoa Al-Ittihad anadai hakuwahi kuomba kusajiliwa kwa Benzema katika klabu hiyo.
0 Comments