Ticker

7/recent/ticker-posts

KAMPUNI KUTOKA CHINA YAONESHA NIA YA KUSAMBAZA UMEME KWENYE VITONGOJI VYA TANZANIA

 

Na Zuena Msuya, DSM

Waziri wa Nishati January Makamba (kushoto) akiongoza kikao kati ya wizara yake na Kampuni ya CMIC kutoka nchini China.

Waziri wa Nishati, January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Kampuni ya vifaa vya Umeme kutoka nchini China (CMI ) iliyoonyesha nia ya kuwekeza katika kusambaza umeme katika  Vitongoji mbalimbali nchini.

Kikao hicho kimefanyika jijini Dar es Salaam, Agosti 7, 2023 kwa kuwashirikisha viongozi wakuu wa Wizara akiwemo Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga, na viongozi wengine kutoka taasisi zilizo chini ya wizara hiyo ambazo ni Wakala wa Nishati Vijijii (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).Katika kikao hicho, Waziri Makamba ameieleza kampuni hiyo kuwa wizara yake iko tayari kufanya kazi nao kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme nchini ikiwemo ushindani wa zabuni.

Aidha amewaeleza kuwa fursa za uwekezaji nchini ziko wazi na serikali imeweka mazingira rafiki na rahisi kwa wawekezaji kuwekeza nchini.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya CMIC, Li Guangyin ameshukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati kwa ushirikiano walioonyesha pamoja na kukubali kufanya mazungumzo na kampuni yake juu ya nia yao ya kusambaza umeme katika vitongoji.

 

  


Post a Comment

0 Comments