Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba leo wametia saini mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 30 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 69.9 za Tanzania.
Utiaji saini huo ulimuhusisha Dkt. Nchemba na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (Abu Dhabi Fund for Development), Mohammed Saif Al Suwaidi.
Fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa Msongo wa kV 220, yenye urefu wa kilometa 167 kutoka Benaco hadi Kyaka, pamoja na Upanuzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kyaka mkoani Kagera.
Tukio hilo pia limeshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Tanzania na Mfuko huo, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Balozi wa Tanzania-Falme za Nchi za Kiarabu-Luteni Jenerali (Mstaafu) Yacoub Hassan Mohammed, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango huo, Lawrence Mafuru, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Maharage Chande, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Rished Bade, Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Japhet Justin, pamoja na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania UAE.
0 Comments