Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amelalamikia namna ambavyo klabu za Saudi Arabia zinamwaga pesa kwa ajili ya kusajili wachezaji.
Klopp ameenda mbali na kusema, anguko la klabu za Ulaya linaanza kutengenezwa na Ligi ya Saudi Arabia. Ameomba UEFA na FIFA kutafuta suluhu ya hili jambo.
Kitu kingine anacholalamikia Klopp ni dirisha la usajili Saudi Arabia kufungwa mwezi Septemba 20 wakati nchi nyingi za Ulaya madirisha ya usajili yanafungwa Septemba 1.
Anachokiona Klopp ni kwamba, wakati dirisha la usajili Ulaya limefungwa, Saudi Arabia watakuwa bado wanaweza kusajili! Hofu yake ni klabu za Saudi Arabia bado zitaweza kusajili wachezaji kutoka Ulaya.
Kwa hiyo wakati makocha wa klabu za Ulaya wakiwa wanaamini kikosi chake ni hiki kwa ajili ya msimu husika, inawezekana sasa klabu za Saudi Arabia zikachomoa wachezaji Ulaya kwa sababu dirisha lao la usajili litakuwa wazi.
0 Comments