Ticker

7/recent/ticker-posts

​EM HOSPITAL YAANZA RASMI KUTOA HUDUMA YA KUSAFISHA FIGO


Hospitali mpya na ya kisasa ya EM Hospital iliyopo,Mji Mwema,  Kigamboni jijini Dar es Salaam, sasa imeanza rasmi kutoa huduma  za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo ( haemodialysis).

Hayo yamebainishwa mapema wiki hii na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dkt. Egina Makwabe.

Dkt. Makwabe ameeleza kuwa EM Hospital imejipanga vizuri kutoa huduma hiyo kwa kuwa vifaa vya kisasa pamoja na wataalamu waliobobea katika utoaji wa huduma hiyo.


Mbali kutoa huduma bora ya kusafisha damu pia inatoa huduma ya upasuaji wa kisasa bila kupasua tumbo.

Aidha Hospitali hiyo inapolea Bima zote kwa ajili ya kutoa matibabu kwa wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.


Post a Comment

0 Comments