Ticker

7/recent/ticker-posts

GARI LA MAFUTA LATEKETEA KWA MOTO KIMARA

Asubuhi ya leo Agosti 6,2023 ilikuwa ya msuko msuko kwa baadhi ya wakazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, baada ya kushuhudia gari la kubeba mafuta likiteketea Kwa moto. 

Taharuki ajali hiyo imetokea kwa wakazi wa maeneo ya Kimara eneo la Kibo barabara ya Morogoro.

Ghafla  gari hilo lililipuka na kuibua mkubwa ulioambatana na moshi.

Walioshuhudia wameeleza kuwa  katika ajali hiyo ya moto, ndani ya gari ya kubeba mafuta kulikuwa na abria watatu, wawili walifanikiwa kutoka na mmoja hajaonekana, hivyo haijulikani kama ametoka akiwa hai au ameteketea kwa moto. 

Mashuhuda hao wameeleza kuwa

moto huo ulichukua muda mrefu bila kuzimwa hali iliyosababisha kusambaa katika maeneo mbalimbali ya makazi ya watu na kuanza kuzua taharuki zaidi.

#TAARIFA MKONONI MWAKO.

Post a Comment

0 Comments