Ticker

7/recent/ticker-posts

ZUCKERBERG 'AMCHOKONOA' ELON MUSK

Kampuni ya META wamekuja na mtandao wao mpya unaojulikana kama (Threads) ambao utakuwa na muonekano sawa na mtandao wa (Twitter) ambao unamilikiwa na tajiri namba 1 duniani bwana Elon Musk .

Nadhani utakwenda kuwa moto mkubwa sana kwenye tasnia ya mambo ya tekinolojia kwa mahasimu hawa wa muda mrefu bwana Mark Zuckerberg ambaye ndiye mmiliki wa Kampuni ya META inayomiliki ( Facebook , Whatsapp na Instagram ) 

Mengi yaliyomo kwenye mtandao wa Threads ambao unakwenda kuzinduliwa siku ya Alhamisi kesho kutwa ni kutokuwepo na malipo ama restrictions za aina yoyote kama ilivyokuwa kwenye mtandao wa Twitter Nadhani uhasimu unakwenda kuwa mkubwa baina ya wawili hao ambao kwa lugha rahisi wameweza kulishika soko la tekinolojia kwa kiasi kikubwa sana .


Historia ya hawa vijana ni yenye kufanana baina yao wakati wakiwa katika harakati zao za kutafuta maisha ambapo wote walitokea kwenye ugunduzi wa Program mbalimbali ambazo zilikwenda kuwasaidia watu wengi .

Zuckerberg yeye alifanikiwa katika Facebook na Elon Musk yeye maisha yake yalianzia kubadilika mara baada ya kuunda mtandao wa Paypal kwa mara ya kwanza kabisa miaka ya 1990.

Post a Comment

0 Comments