Ndug.Zitto Zuberi Kabwe
Serikali ihangaike na Mkulima. Mkulima ndio Sura ya Umasikini wa Tanzania.
Sekta ya Kilimo inapaswa kukua kwa kasi ya 6-8% kwa Mwaka ili Pato la Taifa likue kwa 8-10% kwa Mwaka. Tunahitaji kasi hiyo ya ukuaji wa Uchumi kwa Miaka 5 mfululizo ili kuwaondoa kwenye umasikini 60% ya Watu wetu. Tukishikilia ukuaji huo kwa Miaka 10 mfululizo tutafuta umasikini wa kutupwa ( abject poverty) kabisa.
57% ya mchango wa kilimo katika GDP ni sekta ya mazao. Hii ndio LOW HANGING FRUIT! Hapa ndipo pa kufanyia INTERVENTION na kuchochea WHOLE AGRICULTURAL SECTOR ECOSYSTEM.
Tuanze na TIJA! TIJA TIJA TIJA - Mkulima avune mazao mengi zaidi katika ardhi anayolima sasa.
Mchango wa shughuli ndogo za mazao katika Pato la Taifa (GDP) ni 15%. Shughuli za mazao zilikua kwa 2.7% tu Mwaka 2022. Shughuli hii ya Uchumi Ndio yenye Watanzania wengi zaidi na Ndio njia ya haraka kuwatoa Watu kwenye umasikini.
Watunga Sera waweke Mkakati wa kuongeza TIJA ( productivity) katika shughuli hii.
Kwa Mfano
- Mkulima wa Mahindi azalishe gunia 10/ekari kutoka 4/ekari ilivyo sasa.
- Mkulima wa Pamba azalishe kilo 800-1000/ekari kutoka kilo 150-200/ekari ilivyo sasa.
Kwenye kila zao tumwezeshe Mkulima kuongeza Tija katika kipande Chake cha ardhi anacholima hivi sasa. Hii peke yake itaongeza uzalishaji wa chakula mara 2 ya sasa, vile vile uzalishaji wa mazao ya Biashara mpaka mara 5 ya sasa na kuwezesha Nchi kupata Fedha nyingi za kigeni.
Tufanye nini
1. Serikali ifanye kazi kubwa ya mawasiliano na Wakulima ( Behaviour Change Communications ) hususan kuhusu mbinu za kuongeza tija na masoko. Turudi Enzi za vipindi vya ‘Mkulima wa Kisasa’ kwa kutumia njia za kisasa za mawasiliano. Mawasiliano! Mawasiliano! Mawasiliano!
2. Serikali itoe motisha kwa Wakulima wanaofanya vizuri kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka Taifa. Mfano wakulima bora wa kila Kata nchini wakutane na Rais Kila Mwaka wakati wa wiki ya Wakulima na wapewe zawadi. Zoezi la Usajili wa Wakulima litasaidia sana hii kwani itakuwa rahisi kuwa na rekodi za uzalishaji wao.
3. Huduma za ugani kwa Wakulima ziimarishwe na maafisa ugani wanaofanya vizuri wapewe motisha na wanaofanya vibaya waadhibiwe. Tasnia ya uafisa ugani itazamwe namna inaweza kuwa huru yaani maafisa ugani Binafsi watambuliwe Rasmi.
4. NFRA iendelee kuongezewa uwezo wa kifedha na teknolojia ili itoe uhakika wa Soko la mazao ya chakula kwa Wakulima na vile vile uhakika wa ugavi wa chakula kwa walaji. Benchmark ya Hifadhi ya Chakula ya kutosha miezi 3 ( Mahindi tani 1.5M, Mchele tani 300,000, Maharage, Mtama, Uwele nk ) Itahakikisha kuwa angalau 25% ya chakula kinachozalishwa kinanunuliwa na NFRA.
5. Kwa kupitia Usajili wa Wakulima nchini, Skimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima inaweza kuanzishwa ili kuwezesha wakulima kuweka Akiba, kupata Fao la Bei na Bima ya Afya na uhakika wa Maisha ya uzeeni ( pensheni ). 6. Serikali iimarishe Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kwa kuiwezesha kushiriki katika Biashara ya kwanza usambazaji wa mbolea na baadaye uzalishaji wa mbolea. Kwa kutumia Usajili wa Wakulima, kila Mkulima apate mbolea kwa wakati na aina sahihi ya mbolea.
7. Serikali ibadili muundo wa Bodi za Mazao ili zitimize wajibu wao kwa ufanisi. Bodi za mazao zisiwe wanyonyaji wa wakulima bali wawezeshaji wa wakulima. Vyama vya wakulima viwe na Uwakilishi mkubwa kwenye Bodi za Mazao, Uwakilishi wa kupigiwa kura na wakulima wenyewe.
8. Tuimarishe sana ushirika. Vyama vya Msingi na Vyama Vikuu viwe vyombo vya Kidemokrasia na viendeshwe kwa matakwa ya wakulima wenyewe. Vyama vya Ushirika viwe vituo rejea vya Maendeleo ya wakulima. Serikali isiingilie uendeshaji wao na vile vile wakulima wasilazimishwe kujiunga. Ushirika ushindane na Sekta Binafsi ili kuongeza ufanisi. Wakulima wakiona matunda ya ushirika wataimarisha ushirika. Turudi nyuma kujifunza (rejea Ruvuma Development Association (RDA))!
9. Rudia kusoma namba 1
10. Rudia kusoma namba 1
Marrakesh, Morocco
16/07/2023
0 Comments