Waandishi wa Havari za Mazingira waliofanya ziara ya mafunzo kwenye Eneo la Wanyamapori la Makuyuni,wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa TAWA |
Waandishi wa Habari za Mazingira walio chini ya mwamvuli wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) jana April 30, 2024, walifanya ziara ya mafunzo kwenye Hifadhi ya Wanyamapori ya Makuyuni, iliyopo Monduli mkoani Arusha yenye lengo la kujifunza namna sahihi ya uhifadhi wa Maliasili.
Mbali na mafunzo hayo, lakini pia waandishi hao takribani saba walipata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo ndani ya hifadhi hiyo.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa mafunzo na utekelezaji wa mradi wa Tuhifadhi Maliasili unaoratibiwa na JET kwa ufadhili wa shirika la Misaada la Marekani (USAID), itakumbukwa kuwa kundi hilo la Waandishi wa Havari ni miongoni mwa zaidi ya Wanahabari 20 waliopatiwa mafunzo ya awali ya uandishi wa Haberi zenye lengo la kuokoa shoroba.
Mafunzo ya awali yalifanyika Bagamoyo mkoani Pwani mapema mwaka huu, ambapo waandishi wa Havari za Mazingira walipewa mafunzo mbalimbali na wataalamu wa masuala ya Uhifadhi.
Mradi huo umelenga kuokoa shoroba za wanyamapori zilizoathiriwa na shughuli za binadamu.
Makuyuni ni sehemu ya ushoroba wa Ziwa Manyara/Tarangire ambao unastahili kuwekewa nguvu kubwa ya kuikoa kutokana na kuongezeka kwa kasi ya shughuli za binadamu.
Waandishi waliofanya ziara hiyo wametoka katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Clouds TV na Redio, magazeti ya Nipashe, Zanzibar Leo, Daily News na The Guardian.
Hifadhi ya Wanyamapori ya Makuyuni imebarikiwa aina mbalimbali za wanyamapori wakiwemo twiga, pundamilia, pofu, nyati, ngiri, swala, tembo, pamoja mbalimbali baadhi yao ni kanga, tumbusi na njiwa.
0 Comments