Ticker

7/recent/ticker-posts

YANGA YATIMIZA AGIZO LA RAIS, FEISAL SASA KWENDA AZAM FC

Uongonzi wa Yanga umefikia makubaliano na Feisal Salamu rasmi kwa kuachana kwa amani baada ya kumaliza mazungumzo yao leo.

Yanga wamekubali kumuuza Feisal Salumu kwenda kwa klabu ya Azam Fc kwa dau la Tshs 270.4m kiasi ambacho Yanga sc walikiomba Kutoka kwa Azam Fc kununua mkataba wake Kwenye mazungumzo yao hapo jana.

Awali hapo jana Azam Fc walifikia dau la 160M lakini Yanga waliligomea dau hilo na kuwalazimu klabu ya Azam Fc kurudi tena na ofa yao leo ya pili.

Yanga itapokea kiasi cha 150M mwishoni mwa mwezi huu kama ada ya awali ya usajili kutoka kwa Azam fc na baadae Azam Fc watamalizia  kiasi kilichobaki cha 120.4m katikati ya mwezi Julai mwaka huu.


Kwenye suala hilo  hakuna makubaliano yoyote kati ya Yanga na Azam Fc  ambalo litamuhusisha kiungo Akaminko kama sehemu ya dili hili kama Yanga walivyotaka kumjumuisha kiungo Akaminko.

Hivyo ni rasmi muda wowote kuanzia sasa Yanga itatoa taarifa kwa umma juu ya taarifa rasmi ya kuachana na Feisal Salamu.

Kinachoendelea kwa sasa ni makubaliano ya kimkataba kati ya uongozi wa Yanga na uongozi wa Azam Fc pamoja na menejimenti ya Feisal Salumu juu ya malipo ya ada ya usajili.

Mara tu baada ya kumalizika kwa makubaliano haya Feisal Salumu atakuwa huru kujiunga na Azam Fc.

Post a Comment

0 Comments