Ticker

7/recent/ticker-posts

​TLS YASEMA KIFUNGU CHA 21 CHA MKATABA WA BANDARI KINA UKINZANI WA KISHERIA

 

Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS)  kimebaini ukinzani wa kisheria katika mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji na uboreshaji bandari ya Dar es Salaam kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World.

Sababu ya  ukinzani huo, kwa mujibu wa TLS ni katika kifungu cha 21 cha mkataba huo kinachotaka sheria zitakazoongoza ni zile za Uingereza ilhali Serikali mwenyeji wa makubaliano ya mradi ni Tanzania.

Katika taarifa yake iliyoitoa leo, Juni 26, 2023 TLS imesema imebaini kifungu hicho kinasababisha mgongano wa kisheria kati ya pande zilizokubaliana.

Ni vigumu mradi unatekelezwa Tanzania lakini ukaongozwa kwa sheria za Kiingereza,” imeeleza taarifa hiyo.

Kutokana na hilo, TLS imependekeza marekebisho katika kifungu hicho, ikitaka sheria za Tanzania ndizo zitumike kuongoza mkataba huo.

“Hili linaweza kutekelezwa kupitia Kifungu cha 22 cha mkataba, mara baada ya uidhinishaji mchakato kukamilika ambapo mabadiliko ya vyombo vya uidhinishaji unafanyika kulingana na Kifungu cha 25(4),” imesema.

Imesema sheria ya Kiingereza na Tanzania zinatofautiana katika suala haki ya umiliki wa ardhi kwani ya Tanzania mgeni hawezi kumiliki ardhi kama inavyotakiwa na Sheria ya Ardhi ya Uingereza.

“Kulingana na sheria za Tanzania mgeni anamiliki ardhi kwa madhumuni ya uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),” imesema.

Pasi na kurekebishwa hilo, TLS inasema kutakuwa na mgongano wa sheria.

Post a Comment

0 Comments