Sakata la mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa Bandari nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya DP World limewaingiza hatiani vijana waliokuwa wakiandamana kuupinga
Tayari jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana hao waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba huo.
Mratibu wa maandamano hayo, Deus Soka aliwaacha solemna vijana aliowahamasisha kuandamana.
Maandamano hayo yalipangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Juni 15 mwaka huu Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba huo.
Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.
Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.
Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.
0 Comments