Ticker

7/recent/ticker-posts

KOCHA YANGA HAPENDI MAZOEZI YA KUMKIMBIZA MCHEZAJI NI YA KIZAMANI

Kocha wa viungo wa Yanga, Helmy Gueldich amesema mazoezi ya kumkimbiza mchezaji yamepitwa na wakati na sasa mchezaji anatakiwa kufanya mazoezi ya kuuchezea mpira zaidi.

Helmy anasema suala hilo lilikuwa gumu kwa wachezaji wake, lakini angalau sasa kila mchezaji amemuelewa.

“Nilipoanza Yanga kitu kikubwa kigumu kilikuwa kuwakataza wachezaji kukimbia sana mbio inaonekana hiki kilikuwa vichwani kwao kwamba ili uwe fiti unatakiwa kukimbia sana lakini mazoezi ya kisasa hayataki mbio hizo bila mpira mchezaji wa soka anatakiwa kufanya mazoezi ya kukimbia akiwa na mpira.

“Mchezaji wa kisasa anatakiwa kitu cha kwanza kikubwa afanye mazoezi ya gym haya hayaepukiki ni lazima yafanyike, kitu cha pili unatakiwa kufanya mazoezi ya fiziki na sio kukimbia hawa sio watu wa riadha, kwahiyo kama mnakimbia kwa mbio fupi wanatakiwa kukimbia na mpira sio bila mpira, baadaye mtapiga mashuti au mtafanya mazoezi ya kupiga vichwa mpira, hili lilikuwa gumu sana kukubalika kwa kuwa ilikuwa mpya ila sasa kila mtu ameelewa.” Helmy Gueldich.

Post a Comment

0 Comments