Hanaa Mohamed Hassan(29) kutoka nchini Misri ambaye mwezi uliopita alimuua mwanae wa miaka mitano kwa kutumia sime kisha kumkatakata vipande, kupika sehemu ya kichwa chake na kumla nyama mwanae, ripoti mpya ya uchunguzi imetoka sasa ambapo mwendesha mashtaka amesema mama huyo hakuwa na matatizo ya akili wakati anatenda kosa husika, hakunywa dawa wala hakuwa katika matibabu ya dawa kuwa labda ndizo zilisababisha kutenda unyama kwa mwanae
Sababu ya kutenda unyama ripoti imesema ni mgogoro wa kifamilia kati ya yeye na mumewe baba wa mtoto wake ambaye waliachana miaka minne iliyopita
Baba wa mtoto amesema Hanaa alikuwa anamiliki ardhi toka kwa baba yake hivyo kumtaka mumewe waondoke walipokuwa wakiishi na familia ya mume waenda huko kwenye ardhi anayoimiliki mke. Baba mtoto alikataa kuondoka walipokuwa wakishii kuiacha familia yake hivyo wakaamua kuachana kwa talaka ambapo Hanaa ndie aliyetaka iwe hivyo waachane
Walipeana talaka na mwanaume akawa anahakikisha anaenda muona mtoto mara kwa mara na kumpelekea mahitaji mtoto zikiwemo nguo, baadaye mume akataka waliyamalize na mama mtoto wake ila mama mtoto alikuwa na msimamo wake ule ule hakutaka kingine kiendelee baina yao
Hanaa aliona kama usumbufu baba mtoto kumfuata mara kwa mara kutaka kumuona mtoto, baba mtoto anasema Hanaa alianza kupandikiza chuki kwa mtoto amchukie baba yake
Mwishowe Hanaa akataka uhuru zaidi na mwanae ndio akamuaa mwanae na kumla nyama kwa madai amefanya hivyo kwakuwa anampenda sana mwanae alitaka abaki nae milele
Hukumu bado kutolewa.
0 Comments