Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Leo Juni 5,2023 imehitimisha rasmi mgogoro wamuda mrefu uliomuhusisha mchezaji Feisal Salum na uongozi wa Yanga.
Rais Dkt. Samia ameutaka uongozi wa klabu ya Yanga kuhakikisha wanakaa mezani na mchezaji huyo ili kumaliza tofauti zao.
"Viongozi wa Yanga nami nina ombi kwenu, sifurahii mnavyogombana na wachezaji wenu.
"Hebu kaangalieni namna mtakavyolimaliza hili, sioni sababu Kwa klabu nzuri na bora kama hii kugombana na katoto kale. Kamalize na mje mnipe mrejesho mapema..."
Rais ameyasema hayo leo Ikulu,jijini Dar es Salaam, katika hafla maalum ya kuipongeza Yanga baada ya kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Shiriksho Barani Afrika.
Feisal ndio alikuwa wa kwanza kuuibua mgogoro huo akidai kuboreshewa maslahi.
Mara kadhaa Feisal alilipeleka shauri lake TFF lakini alijikuta akiangukia pua baada ya kushinda na kuamriwa kurejea kuitumikia Yanga.
Uamuzi huo ulimfanya Fei kulipeleka suala lake CAS.
0 Comments