Jeshi la Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imepanda miti zaidi ya 17,000 ili kuilinda na upepo mkali Ikulu mpya ya Chamwino, jijini Dodoma inayotarajia kuzinduliwa rasmi kesho na Rais Dkt. Samia Sulubu Hassan.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa jeshi hilo Kanda ya kati, Kamishna Msaidizi mwandamizi Mathew Kiondo leo.
Kamanda Kiondo amesema, Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) wamepanda zaidi ya miti 17,000 kwenye ardhi ya Ikulu huku baadhi ya miti ikiwa na sifa ya kuzuia upepo mkali unaovuma katika mkoa huo wa Dodoma.
Aidha Kamanda Kiondo ameongeza kuwa eneo kubwa la ardhi ya Ikulu hiyo imepandwa miti yenye kuleta kivuli na matunda na miti ya kupendezesha mandhari ya Ikulu.
Ikulu hiyo mpya iliyoanza kujengwa na serikali ya Awamu ya Tano, ambayo iko Chamwino jijini Dodoma inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho Mei 20, 2023 na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
0 Comments