Ticker

7/recent/ticker-posts

SASA YANGA HAIZUILIKI, MAYELE KAMA KATAPILA

Ni wazi sasa hakuna timu inayoweza kukizuia kikosi Cha Yanga kisijikusanyie mataji mamubwa ya soka Tanzania Bara msimu huu.

Tayari Yanga imeshanyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na michezo miwili mkononi na pointi saba zaidi ya timu ya Simba inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Mbali na kutetea ubingwa wake wa  Ligi Kuu, lakini pia iko kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Kama hayo hayatoshi tayari leo  imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Yanga ikiwa na kikosi kilichoundwa na wachezaji wengi wasiopata nafasi  kweye kikosi cha kwanza, imeweza kuitandika  Singida Big Stars bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja  wa Liti mkoani Singida.

Kupewa nafasi ya kuanza Kwa Mauya, Doumbia, Mzize na mlinda lango Metacha Mnata kulidhihirisha wazi kuwa sasa Yanga ina kikosi kipana.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kuvutia timu zote  zilitengeneza nafasi za magoli katika kipindi cha kwanza bila mafanikio, Hali iliyowapeleka  mapumziko wakiwa 0-0.


Yanga ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake walioanza na kuwapa nafasi Fiston Mayele, Tuisila Kisinda, Dikson Job na Musonda.

Mabadiliko hayo yalizaa matunda, ambapo kikosi cha Singida kilianza kusakamwa na Yanga kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Mayele na matokeo kuwa 1-0 hadi mwisho wa mchezo.

Yanga Sasa imeenda fainali na itakutana na Azam Fc  iliyotinga kwenye hatua hiyo baada ya kuichapa Simba 2-1.

Fainali hiyo imepangwa kuchezwa  katika dimba la Mkwakwani jijini, Tanga.

Post a Comment

0 Comments