Mnamo Mei 21 Mwaka - 1996 meli ya abiria na mizigo ya MV Bukoba, ilipata ajali.
Hii ni ajali ya kihistoria, pengine ni moja ya ajali iliyoua watu wengi zaidi kwa wakati mmoja kuwahi kutokea Tanzania katika miongo ya hivi karibuni. Ilitokea Mei 21, 1996, na hata Serikali iliwahi kukiri kwamba ajali hiyo itaendelea kuwa miongoni mwa kumbukumbu mbaya kutokana na kuangamiza maisha ya mamia ya Watanzania wengi kwa wakati mmoja.
Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 800 walifariki katika ajali hiyo iliyotokea kilomita chache kutoka bandari ya Mwanza.
Ingawa ni miaka 27 sasa tangu kuzama kwa meli ya MV Bukoba, Bukoba ilipokuwa inakaribia bandari ya Mwanza umbali wa kilometa 56, aliyekuwepo na asiyekuwepo historia yake imeendelea kukaa vichwnai mwa wengi.
Meli hiyo iliyoundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 iliyokuwa tegemeo kubwa la kutoa huduma ya kubeba mizigo na abiria ndani ya Ziwa Victoria kati ya Bandari za Bukoba na Mwanza. Siku ya ajali inaelezwa kupakia zaidi ya abiria 2,000.
0 Comments