Ticker

7/recent/ticker-posts

UVCCM UBUNGO YAWATAKA VIJANA KUTUMIA KIMWANGA CUP KUELEZA MAFANIKIO YA SERIKALI YA RAIS DKT.SAMIA

Na Mwandishi Wetu, Afrinewsswahili

-Dar es Salaam

Vijana wanaoshiriki michuano ya kombe la  Kimwanga  na kombe la Rede la Hawa Abdul, wametakiwa kuyatumia mashindano hayo kujitangaza na kutangaza mafanikio yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Ubungo Shadrack Makangula.

Makangula alitoa rai hiyo kabla ya kuanza kwa mchezo wa nusu fainali uliozikutanisha timu za  Ting Wayland dhidi ya timu ya kituo cha kulea vipaji cha Lamasia FC.

Mchezo huo ulimalizika kwa  Ting kuingia fainali baada ya kushinda  bao 2-0.

Akizungumza na wachezaji na mashabiki waliohudhuria mchezo huo Makangula alisema ni muhimu kwa Vijana kuwa na utayari wa kuzisemea juhudi za Rais Dkt. Samia.

"Yatumieni mashindano haya kuwa mabalozi wa jitahada zinazofanywa na Rais Dkt. Samia katika kuwaletea maendeleo Vijana na wananchi wote wa wilaya ya Ubungo."


Mbali na michuano ya soka ya kuwania Ng'ombe iliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Makurumla Bakari Kimwanga, pia kuna michuano ya  rede iliyoandaliwa na Diwani wa viti maalum Manispaa ya Ubungo, Hawa Abdulrahman.

Kwenye upande wa rede  timu ya Kanuni ilifanikiwa  kwenda fainali kwa ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Manzese Princes.

Michuano hiyo inachezwa kwenye Uwanja wa Bubu Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo.

Mashindano ya rede yanahusisha mabinti ambao pia  mshindi atapata zawadi ya ng’ombe.

Akizungumza zaidi Makangula aliwashukuru   madiwani hao kwa kuona umuhimu mkubwa wa kuanzisha michuano ya mpira wa miguu na rede ambayo yote kwa ujumla wake inawasaidia vijana  kuonyesha vipaji walivyonavyo, lakini pia kupata fursa na kubwa zaidi ni kutengeneza uhusiano mzuri baina ya viongozi na wananchi. 


“Hivyo ni vema kwa mashabiki, wakereketwa na wananchi kwa ujumla ambao timu zao wanazozishabikia zimefuzu kucheza hatua inayofuata   kuhakikisha kuwa wakati michezo hiyo inaendelea wawe na utulivu wawapo uwanjani kwa sababu watakapoanzisha vurugu watawakatisha tamaa wadau, wahisani na viongozi katika kuanzisha ligi mbalimbali kwenye wilaya hiyo.” 

 Mwenyekiti huyo wa UVCCM ametoa msisitizo zaidi Kwa  wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali  ya Awamu ya Sita.


Kutokana na hali hiyo Makangula aliwashukuru viongozi mbalimbali aliombatana nao na kuwaomba madiwani hao wawili wayafanye mashindano hayo kuwa endelevu.

Post a Comment

0 Comments