Kundi maarufu la muziki wa Afro- pop la Sauti Sol lenye maskani yake nchini Kenya sasa limevunjuka rasmi. Tangazo la kuvunjika kwa kundi hilo limetolewa jana Jumamosi, Mei 20, 2023.
Aliyetoa taarifa hiyo ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha kundi hilo, Faarah Nur.
Hata hivyo sababu za kusambaratika kwa kundi hilo hazijawekwa wazi. Katika taarifa hiyo iliyosambazwa kwa vyombo vya habari, walisema kwa kifupi: “Ziara inayokuja ya Marekani, Ulaya na Kanada ni fursa kwa mashabiki kutuona Sauti Sol kwa mara ya mwisho.
Kila onyesho litajazwa na hisia za upendo na shukrani huku bendi ikitumbuiza vibao vya milele na nyimbo zinazopendwa na mashabiki ambazo zimeacha alama isiyofutika kwenye kumbukumbu zetu za pamoja." , walisema wanachama wa kundi hilo.
Sauti Sol liliundwa mwaka 2005 likiunganisha vijana wanne machachari watatu wakiwa waimbani na muungano wa Moja mpiga gitaa.
Vijana hao ni Bien-Aimé Baraza, Willis Chimano na Savara Mudigi ambao walikuwa ni waimbani na mpiga gitaa alikuwa ni Polycarpe Otieno.
Kundi hilo lilitoa albamu yake ya kwanza mwaka 2008 iliyojulikana kwa jina la Mwanzo.
Albamu ya pili walitoa mwaka 2011 ikiwa na jina la Sol Filosofia. Mwaka 2015 waliachia albamu ya tatu iliyobeba jina la Live and Die in Afrika na mwaka 2020 kundi lilirejea na albamu ya nne na ya mwisho.
Kundi hili lilionesha ubora mkubwa kuanzia kutunga wimbo, kutengeneza na kuimba kwa pamoja.
Hili lilikua miongoni mwa makundi bora barani Afrika ma duniani kwa ujumla
0 Comments