Hayati Bernard Kamilius Membe alikuwa ni miongoni mwa machifu watatu wa kabila la Wamwera.
Hata sababu ya mwili wake kupokelewa na wazee imetokana na hadhi yake ya uchifu.
Hayo yamebainishwa na kiongozi wa kimila wa kabila la Wamwera, chifu Nakote Ismail Malibiche wa Ilulu, Nachingwea.
Wazee wa kimila jana walioupokea mwili wa Membe na kuufanyia tambiko, lengo likiwa ni kumpa heshima zake.
Chifu Nakote alisema kwa kawaida mtu anapewa uchifu Kwa kurithi kulingana na historia ya ukoo wake kuwa na chifu.
Hata hivyo Membe hakutokea kwenye ukoo WA chifu isipokuwa amesimikwa uchifu wa heshima baada ya Wana Rondo kuwa na furaha ya kumpata kiongozi wa juu katika serikali jambo ambalo halikuwahi kutokea.
Membe amezikwa leo kijijini kwao.
0 Comments