WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na Mitaala Toleo la 2023, imewataka wadau kutoa maoni, kuhusu rasimu hiyo kwa kuwa umri wa kuanza darasa la kwanza utakuwa miaka sita badala ya saba.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda. amesema rasimu hiyo, inapendekezwa umri wa kuanza ni miaka sita, kama ilivyo katika nchi nyingi duniani huku muundo uliorekebishwa ukiruhusu mwanafunzi kukamilisha mzunguko wa masomo kwa muda wa miaka sita kwa elimu ya msingi.
Muundo katika mfumo rasmi wa elimu na mafunzo utakuwa 1+6+4+2/3+3+, kwa maana ya mwaka mmoja wa elimu ya awali, miaka sita ya elimu ya msingi, miaka minne ya elimu ya sekondari ngazi ya chini, miaka miwili ya elimu ya sekondari ngazi ya juu au miaka mitatu ya amali sanifu na miaka isiyopungua mitatu ya elimu ya juu.
Akizungumza na waandishi jijini hapa, Prof. Mkenda amesema serikali imeamua kutoa rasimu hizo, ili kupata maoni na mwisho wa kuyapokea ni Mei 31, mwaka huu.
0 Comments