Ticker

7/recent/ticker-posts

MWANAFUNZI BUGANDO AJITEKA, AKUTWA GESTI CHUMBA NAMBA 103 AKIBURUDIKA.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha  Afya na Sayansi Shirikishi (CUHAS) cha Bugando, kilichopo mkoani Mwanza, ambaye  jina lake halijajulikana, ameamua kujiteka ili iwe rahisi kutumiwa fedha na familia yake.

Bahati mbaya mbinu yake hiyo ovu haikulishawishi jeshi la Polisi ambalo liliamua kuingia mzigoni kumsaka na ndipo alipokutwa amejituliza ndani ya gesti akila raha.

Inaelezwa nia ya mwanafunzi huyo ilikuwa ni kuwalaghai wazazi wake wamtumie hela ambazo atazitumia kuwapa watekaji wake wa uongo wamuachie.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema, mwanafunzi huyo alijiteka na kukaa kwenye moja ya gesti zilizopoIgongo ndani ya chumba namba 103 huku akisubiri kuitumiwa hela na wazazi wake.

"Alikuwa amepumzika kwenye chumba Cha gesti akila raha zake, baada ya kukamatwa na kuhojiwa alikiri kuwadanganya wazazi wake na viongozi wa chuo kwamba ametekwa Ili apewe fedha zitakazomfanya aendelee kula starehe."

Imeelezwa kuwa katika kuhakikisha kijana wao anaachiwa na watekaji, wazazi walilazimika kuuza baiskeli Ili kupata fedha za kumtumia.

Post a Comment

0 Comments