Ticker

7/recent/ticker-posts

YANGA YAFUNGA HESABU ZA UBINGWA LIGI KUU

Mabingwa wa kihistoria nchini, Yanga SC leo imefunga rasmi hesabu za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kuichapa Dodoma Jiji bao 4-2. 

Ushindi huo umeifanya Yanga kuendeleza rekodi yake ya kutwaa ubingwa mara nyingi sasa ikifikisha  ubingwa wa 29 wa Ligi Kuu Tanzania bara Msimu wa 2022/23. Mchezo wa leo umepigwa kwenye uwanja wa Azam Complex jijini la Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Kennedy Musonda dakika ya 39,Mudathir Yahya akifunga mabao mawili dakika ya 70,90 na Farid Mussa dakika ya 88.

Mabao ya Dodoma jiji yamefungwa na Collins Opare dakika ya 59 na Seif Karihe dakika ya 67.


Ushindi huo unaifanya Yanga SC kutetea tena ubingwa wa Ligi Msimu huu ikiwa imefikisha Pointi 74 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote huku ikiwa imebakiwa na michezo miwili dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons michezo yote itachezwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Post a Comment

0 Comments