Ticker

7/recent/ticker-posts

TSHABALALA ASAKWA AFRIKA KUSINI

Mlinzi wa kushoto wa klabu ya Simba, Mohamed Hussein (Tshabalala) ambae anamaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi mwishoni mwa msimu huu, ameanza kusakwa na  klabu kadhaa za Afrika Kusini na zimeanza kutuma ofa. 

Klabu za Kaizer Chiefs, Royal AM na Orlando Pirates zimetuma ofa rasmi kwa uongozi wa mchezaji huyo huku Supersport United wakimtumia mtu wa kati kufikisha ofa kwa wakala wake.

Aidha Simba pia wameanza mazungumzo na Tshaba ili aongeze kandarasi ambapo kwasasa wanapewa kipaumbele kikubwa kuanzia ofa yao na vipengele vingine vya kimkataba ijapo hajasaini karatasi zozote mpaka hivi sasa. 

Post a Comment

0 Comments