CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepinga kauli ya Makamu Mwenyekiti wake Tundu Lissu kuhusu maridhiano ya chama chao na serikali. Mapema wiki hii akiwa ziarani eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma, Tundu Lissu alisema “Nasikia sikia hivi huko kuwa katika haya maridhiano kuna ahadi ya kuachiana wabunge na kuwa tumeambiwa eti tutapewa majimbo na kuendesha siasa za nusu mkate.” Akizungumza katika moja ya chombo cha habari nchini, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje, John Mrema, amepinga kauli hiyo na kusema suala la kuachiana majimbo halipo kwenye mambo 12 waliyojadiliana na serikali. “Hakuna kitu kama hicho. Suala la kupewa wabunge halimo kwenye mazungumzo ya maridhiano. Tulikuwa na mambo 12 katika maridhiano na serikali. Hilo halimo.” Mwezi Januari mwaka huu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, akiwa jijini Mwanza, aliongelea kuhusu hoja dhaifu za baadhi ya wanachama na viongozi wake wanaopinga maridhiano. Mbowe alisema kuna utofuati mkubwa kati ya uongozi wa Rais Samia na mtangulizi wake Hayati John Pombe Magufuli; na kwamba Rais Samia ameonyesha nia thabiti ya kuleta maridhiano na mshikamano wa kitaifa
0 Comments