Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesitisha zoezi la ukamataji wafanyabiashara wa Kariakoo linalofanywa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) maarufu kama kikosi kazi.
Mbali na hilo pia amesitisha kodi ya stoo kwa muda na kuahidi kuyashughulikia madai mengine ya wafanyabiashara hao waliogoma kufungua biashara leo asubuhi.
“Kamata kamata inayofanywa na vikosi kazi, isitishwe…kodi ya stoo pia isitishwe kwa muda…haya mengine tutaendelea kuyashughulikia…endeleeni na biashara…”
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyasema haya alipozungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo jioni ya leo ambao wamefunga maduka yao tangu asubuhi.
0 Comments