Mmoja wa watuhumiwa wanne wanaodaiwa kumuua aliyekuwa mfanyakazi wa mgodi wa GGM Milembe Selemani amejinyonga. Kwa mujibu wa jeshi la Polisi mkoani Mara, jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wanaodaiwa kufanya mauaji hayo.
Mauji hayo yalifanyika katika mtaa wa Matulole, Kata ya Buhalahala mkoani Geita.
Hata hivyo mtuhumiwa wa nne aliyefahamika Kwa jina la Pastory Lugodisha alijinhonga.
Lugodisha alifanya hivyo baada ya kupata taarifa ya kukamatwa kwa wahalifu wenzake.
Alifanya hivyo kwa kutumia mkanda wa suruali katika pori la hifadhi ya Buhindi Wilayani Sengerema.
0 Comments