Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba wafanyabiashara wa Kariakoo kutofunga maduka yao na kuendelea na biashara ili kulinda heshima na hadhi ya soko hilo.
Amesema uhai wa soko hilo ni biashara, hivyo kama kuna matatizo ni bora shughuli zikaendelea.
“Soko hili kwa uendelevu wake hata kama kuna matatizo bora shughuli zikawa zinaendelea ili tusiendelee kuwapoteza wateja wetu kutoka nje na ile hadhi ya kimataifa iweze kuendelea.” Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo
0 Comments