Thabo Bester |
Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kumfungia kwenye selo yenye ulinzi mkali tapeli la kimataifa maarufu kama mbakaji wa FaceBook, Thabo Bester.
Bester na mpenzi wake Dkt. Nandipa Magumana walirudishwa nchini Afrika Kusini wiki hii wakitokea nchini Tanzania, baada ya kukamatwa na makachero wa jeshi la Polisi jijini Arusha.
Matapeli hao waliweza kutoroka nchini Afrika Kusini na Msumbiji na hatimae kukamatwa Tanzania, ambapo Afrika Kusini iliishukuru Tanzania kwa kufanikisha hilo.
ALITOROKAJE?
Bester alitengeneza kifo cha uongo wakati anatoroka gerezani kwa kuchoma mwili moto kiasi haukutambulika na yeye akatoroka.
Baada ya muda mwanamke, Dkt. Nandipa akajitokeza na kusema kuwa yeye ni mkewe na anataka mwili wa mumewe.
Polisi wakamwambia asubiri maana bado wana kazi na huo mwili.
Polisi wakaufanyia kipimo cha DNA kwa kulinganisha na vinasaba vya mama yake mzazi, majibu yalikuja na kuonesha kuwa mama hafanani na "Marehemu" mtoto wake.
Dkt. Nandipa na Thabo |
Kabla ya kuondoka Afrika Kusini, wakafanya utapeli mkubwa wa kupangisha majumba na utapeli wa mitandaoni huku mumewe akiwa na utambulisho bandia na hati bandia ya kusafiria wakafanikiwa kutoroka Afrika Kusini na kupita nchi kadhaa hadi Tanzania walikokamatwa.
0 Comments