Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amewafurahisha watu wengi kutokana na kauli yake ya kukemea msafara wake kusimamisha watu barabarani kwa saa muda mrefu.Jana Makamu wa Rais, alisema hataki kusikia tena barabara zikifungwa kwa muda mrefu ili kumfanya yeye mtoto wa masikini apite.
Alisema dakika 10 zinamtosha na anahitaji wananchi wawe na uhuru wa kutumia barabara kwa ajili ya kuendelea na shughuli zao.
Dkt. Mpango aliyasema hayo akiwa ziarani jijini Mwanza.
Katika kuonesha uungwana, Makamu wa Rais aliwaomba radhi wananchi kwa kitendo cha barabara kufungwa kwa saa nne ili kumpisha yeye.
"Nilishamwambia IGP na niseme hapa pia kwa makamanda wote wa mikoa, sitaki msafara wangu ufunge barabara kwa muda mrefu, dakika 10 zinanitosha."
Hatua hiyo ya Dkt. Mpango imepongezwa na wengi ambao wanaamini zoezi la kufunga barabara kwa muda mrefu linakera.
0 Comments