Ticker

7/recent/ticker-posts

THAMANI YA MAYELE YAPAA

Matokeo ya bao 2-0 iliyoyapata timu ya Yanga ugenini nchini Nigeria kwenye mji wa Oyo, imepaisha thamani ya mshambuliaji wa mabingwa wa Soka Tanzania, Fiston Mayele.

Mayele ambae kwa sasa ni mshambuliaji hatari ndani na nje ya Ligi Kuu ya NBC, amefainikiwa kuifungia Yanga magoli yote mawili, huku beki kisiki na nahodha wa timu hiyo Bakari Nondo Mwamnyeto akitoa pasi za magoli yote mawili.

Kasi ya ufungaji ya Mayele inamfanya kuongeza thamani yake sokoni, ambapo leo imeiwezesha timu yake kupata alama tatu ugenini.

Matokeo hayo ya ugenini yanaipa nafasi kubwa Yanga kuingia hatua ya nusu fainali, kwani mchezo utakaoamua nani asonge mbele utachezwa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki ijayo.

YANGA IMEFUTA UTEJA

Ukiangalia rekodi kati ya timu hizi mbili, utaona kabisa Yanga anilikuwa ikipewa nafasi ndogo na ilipaswakulipiza kisasi chao cha mwaka 2021 walipokuwa wanasaka tiketi ya kufuzu hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa.

Timu hizi Yanga na  Rivers United zimekutana mara 2 huku mechi zote akishinda Rivers, ikumbukwe kwamba nchini Nigeria Yanga alipoteza kwa bao moja mchezo ukichezwa kwenye dimba la Adokiye Amiesimaka huko Port Harcourt. 

Matokeo ya Leo yameifanya Yanga ya msimu huu kuwa tofauti zaidi na ya misimu miwili nyuma, imeimarika kwenye kila idara kuanzia uwekezaji, benchi la ufundi na wachezaji wenye uwezo mkubwa waliojidhihirisha kwenye mchezo wa leo.

Post a Comment

0 Comments