Ticker

7/recent/ticker-posts

SIMBA KURUDIA YA MWAKA 2003 LIGI YA MABINGWA AFRIKA

TIMU ya Simba jana  imefanikiwa kushinda bao 1-0 dhidi ya  mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika,  Wydad Casablanca ya Morocco.

Simba ilifanikiwa kupata ushindi huo kupitia Kwa mshambuliaji wake Jean Beleke, katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Simba imecheza robo fainali ya kwanza kama ilivyo kwa Al Ahly ya Misri na Raja Casablanca, CR Belouizdad ya Algeria dhidi ya Mamelodi Sundowns na JS Kabylie ya Algeria dhidi ya Espérance ya Tunisia.

Marudiano ya robo fainali ya pili yatachezwa kati ya  Aprili 28 na 29 mwaka huu.

Mshindi kati ya Wydad na Simba atakutana na mshindi kati ya CR Belouizdad ya Algeria na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini 

Simba inaweza kurejea historia yake ya mwaka 2003 ambapo iliwahi kuwatoa mabingwa wa Afrika wa mwaka 2003, Zamalek ya Misri kwa penatii baada ya kila timu kushinda 1-0 nyumbani kwake na mechi ya mwisho ilichezwa Cairo.

Post a Comment

0 Comments