Timu ya Simba ambayo inatajwa kuwa na mashabiki wengi nchini imetinga hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia linaloendelea kwenye mtandao wa Twitter.
Michuano hiyo inaandaliwa na mtandao wa Deportes&Finanzas kutoka Brazil likihusisha klabu zenye wafuasi wengi mitandaoni.
Klabu mbalimbali duniani zimeshiriki kwenye mchezo huo ambao unaendeshwa kwa watu kupiga kura kwa kuichagua timu moja kati ya mbili zilizoshindanishwa.
Simba ni timu pekee inayoshiriki mchezo huo kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.
Juzi Simba ilishindanishwa na Nacional ya Uruguay katika hatua ya 16 bora na kufanikiwa kupata asilimia 65 ya kura huku wapinzani wao wakipata asilimia 35.
Sasa Simba itakutana na River Plate ya Argentina katika hatua ya robo fainali.
0 Comments