Pamoja na kupewa adhabu na klabu yake ya Bayern Munich, mchezaji wa kimataifa wa Senegal, Sadio Mane, ameomba pamoja na kujutia kitendo chake cha kupigana.
Mane akiwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo alimtwanga ngumi mchezaji mwenzake Leroy Sane.
Tukio hilo lilitokea wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Manchester City uliomalizika kwa Buyer kulala kwa 3-0.
Mane ambae pia atatakiwa kulipa faini ataukosa mchezo wa timu yake dhidi ya 1899 Hoffenheim utakaochezwa kesho.
Adhabu hiyo ya Mane inaweza kuwa zaidi ya mechi moja.
Wachambuzi wa soka wanaamini Mane alichukua hatua hiyo baada ya kutolewa maneno ya kashfa na Sane.
0 Comments