Katika halfa ya kuipongeza timu ya wasichana ya shule ya Sekondari Fountain Gate Dodoma ambao ni mabingwa wa Afrika, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewakabidhi mabingwa hao kiasi cha shilingi milioni 5.
Katika hatua nyingine Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikalini za Mitaa imewakabidhi mabingwa hao milioni 3 kama pongezi ya yale waliyofanya katika mashindano ya shule za Sekondari barani Afrika.
Ikumbukwe juzi mabingwa hao walipewa milioni 10 na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Fedha hizo zinakwenda moja kwa moja kwa wanafunzi hao na benchi la ufundi ikiwa ni sehemu ya zawadi na pongezi baada ya kuiingizia taasisi yao zaidi ya million 800 na kuwapatia ubingwa kwenye mashindano ya African Schools Football Championship kuanzia hatua ya Ukanda wa CECAFA na Afrika.
0 Comments